Utusaidie kukuza uelewa wa pamoja kuhusu jinsi tunavyoweza kushirikiana ili kusaidia wanafunzi wote katika safari yao ya kujifunza.

Hii inahusu nini?

Idara ya Elimu ya NSW inataka maoni kutoka wazazi, walezi na wafanyakazi kuhusu kile ambacho ni muhimu, tunachopaswa kuendeleza na jinsi tunavyoweza kuwezesha uzoefu thabiti na wa hali ya juu kwa wazazi na walezi wote wa watoto na vijana, na wafanyakazi katika elimu ya umma.

Wazazi na walezi ni mwalimu wa kwanza wa mtoto wao. Kushirikisha na kujifunza kwa mtoto wao huanza kutoka utoto wa mapema na huendelea kupitia hatua tofauti za maendeleo na mazingira ya kujifunza. Hii inaweza kuhusisha kusaidia elimu, maendeleo na ushiriki wa mtoto wao, kutafuta njia za kuleta elimu nyumbani, na kusaidia walimu na wafanyakazi kumjua na kumwelewa mtoto wao.

Tunajua ushirikiano thabiti katika jumuiya za elimu, kati ya wanafunzi, wazazi na walezi, walimu, waelimishaji, wafanyakazi wa shule na wa idara, husaidia kukuza ushiriki na matokeo mazuri ya kujifunza na ustawi.

Maoni yako yatasaidia kuunda mfumo wa ushiriki wa mzazi na mlezi. Tunataka kuwasaidia wazazi na walezi:

  • kuelewa kwa uwazi haki, majukumu na uchaguzi wao kuunga mkono elimu ya mtoto wao

  • kupata habari rahisi kueleweka na kwa wakati ili kuwasaidia kuunga mkono na elimu, maendeleo na ustawi wa mtoto wao

  • kutoa maoni yako katika mambo yanayoathari elimu ya mtoto wao, na kuona matokeo yanayoonyesha ushiriki wao

  • kujiamini katika kueleza wasiwasi wake au kujua jinsi ya kutoa malalamiko ambapo hawajaridhika na sehemu ya elimu ya mtoto wao

  • kupokea huduma na usaidizi unaotarajia mahitaji na kukidhi utofauti

  • kushiriki na elimu ya mtoto wao, kuungwa mkono na ushirikiano thabiti na wafanyakazi ili kufikia malengo ya pamoja

Toa maoni yako

Tunakaribisha maoni yako, kama

  • wazazi au walezi wanaosaidia elimu na ujifunzaji wa mtoto wako, au,

  • wafanyakazi wa idara, kufanya kazi na jumuiya yako.

Tunataka kusikia nini ni muhimu kwako na unaweza kushiriki kwa njia nyingi upendavyo kuchagua. Tarehe ya mwisho kushiriki ni tarehe 30 Aprili 2022.

Utafiti

CLOSED: This survey has concluded.

Mazungumzo

CLOSED: This discussion has concluded.

Njoo kujiunga mazungumzo: Kujihusisha kuna maana gani kwangu? Mtindo huu unadokeza kuna njia 3 muhimu za kujihusisha.

Ili kutazama picha iliyopanuliwa, bonyeza kulia kwenye picha na chagua ‘Fungua picha kwenye kichupo kipya’

Kujihusisha kuna maana gani kwako?

Je, kuna njia nyingine za kushiriki ambazo hazipo kutoka mtindo huu?

Kwa maslahi ya faragha au siri, tunakuomba usitamke jina la shule au mtoaji wa ujifunzaji, walimu, wafanyakazi, wanafunzi wowote au watu wengine unaposhiriki maoni yako. Maoni ambayo yanawezekana kukashifu hayatavumiliwa na yataondolewa na wasimamizi wetu. Asante

Utahitaji kujiandikisha kwanza ili kujiunga na mazungumzo.

Mawazo

CLOSED: This activity has concluded.

Shiriki mawazo yako: Nini ni muhimu kwako? Unataka kujihusisha kuhusu nini?

Ili kutazama picha iliyopanuliwa, bonyeza kulia kwenye picha na chagua ‘Fungua picha kwenye kichupo kipya’

Ukifikiria kuhusu uzoefu wako wa kujihusisha ili kumsaidia mtoto katika elimu yake, unataka nini:

  • Kujua kuhusu nini?
  • Wengine kujua kuhusu nini?
  • Kufanya maamuzi kuhusu nini?

Kwa maslahi ya faragha au siri, tunakuomba usitamke jina la shule au mtoaji wa ujifunzaji, walimu, wafanyakazi, wanafunzi wowote au watu wengine unaposhiriki maoni yako. Maoni ambayo yanawezekana kukashifu hayatavumiliwa na yataondolewa na wasimamizi wetu. Asante

Utahitaji kujiandikisha kwanza ili kushiriki mawazo yako.

Hadithi yako

CLOSED: This discussion has concluded.

Tuambie hadithi yako: tunaweza kufanyaje ili kushiriki kutakuwa tukio zuri?

Ukifikiri wakati ulipotaka au kuhitaji kujihusisha kusaidia elimu ya mtoto:

  1. Ulitaka kujihusisha kuhusu nini?
  2. Eleza ni nini kilichotokea kupitia kushiriki
    • tambua pointi ambazo zilikuwa nzuri au mbaya
    • pointi zile kutoka picha hapo juu zinaweza kukusaidia kueleza uzoefu wako
  3. Nini ingeweza kutokea katika siku za usoni
    • Kuboresha hii; na/au
    • Kuendelea kutoa uzoefu mzuri

Kwa maslahi ya faragha au siri, tunakuomba usitamke jina la shule au mtoaji wa ujifunzaji, walimu, wafanyakazi, wanafunzi wowote au watu wengine unaposhiriki maoni yako. Maoni ambayo yanawezekana kukashifu hayatavumiliwa na yataondolewa na wasimamizi wetu. Asante

Utahitaji kujiandikisha kwanza ili kushiriki hadithi yako.