Kuwashirikisha wazazi na walezi katika elimu ya mtoto wao
Utusaidie kukuza uelewa wa pamoja kuhusu jinsi tunavyoweza kushirikiana ili kusaidia wanafunzi wote katika safari yao ya kujifunza.
Hii inahusu nini?
Idara ya Elimu ya NSW inataka maoni kutoka wazazi, walezi na wafanyakazi kuhusu kile ambacho ni muhimu, tunachopaswa kuendeleza na jinsi tunavyoweza kuwezesha uzoefu thabiti na wa hali ya juu kwa wazazi na walezi wote wa watoto na vijana, na wafanyakazi katika elimu ya umma.
Wazazi na walezi ni mwalimu wa kwanza wa mtoto wao. Kushirikisha na kujifunza kwa mtoto wao huanza kutoka utoto wa mapema na huendelea kupitia hatua tofauti za maendeleo na mazingira ya kujifunza. Hii inaweza kuhusisha kusaidia elimu, maendeleo na ushiriki wa mtoto wao, kutafuta njia za kuleta elimu nyumbani, na kusaidia walimu na wafanyakazi kumjua na kumwelewa mtoto wao.
Tunajua ushirikiano thabiti katika jumuiya za elimu, kati ya wanafunzi, wazazi na walezi, walimu, waelimishaji, wafanyakazi wa shule na wa idara, husaidia kukuza ushiriki na matokeo mazuri ya kujifunza na ustawi.
Maoni yako yatasaidia kuunda mfumo wa ushiriki wa mzazi na mlezi. Tunataka kuwasaidia wazazi na walezi:
kuelewa kwa uwazi haki, majukumu na uchaguzi wao kuunga mkono elimu ya mtoto wao
kupata habari rahisi kueleweka na kwa wakati ili kuwasaidia kuunga mkono na elimu, maendeleo na ustawi wa mtoto wao
kutoa maoni yako katika mambo yanayoathari elimu ya mtoto wao, na kuona matokeo yanayoonyesha ushiriki wao
kujiamini katika kueleza wasiwasi wake au kujua jinsi ya kutoa malalamiko ambapo hawajaridhika na sehemu ya elimu ya mtoto wao
kupokea huduma na usaidizi unaotarajia mahitaji na kukidhi utofauti
kushiriki na elimu ya mtoto wao, kuungwa mkono na ushirikiano thabiti na wafanyakazi ili kufikia malengo ya pamoja
Toa maoni yako
Tunakaribisha maoni yako, kama
wazazi au walezi wanaosaidia elimu na ujifunzaji wa mtoto wako, au,
wafanyakazi wa idara, kufanya kazi na jumuiya yako.
Tunataka kusikia nini ni muhimu kwako na unaweza kushiriki kwa njia nyingi upendavyo kuchagua. Tarehe ya mwisho kushiriki ni tarehe 30 Aprili 2022.